Fursa Za Kifedha Katika Ufugaji
Elimu ya fedha na fursa za kilimo-biashara na ufugaji nchini Tanzania.

03–04 Oktoba 2026 · Dar es Salaam
Semina ya siku mbili kwa wafugaji, wawekezaji, vijana na wadau wanaotaka kubadili ufugaji kuwa biashara yenye tija, iliyoandaliwa na Wafugaji Pwani kwa uratibu wa Mount Nebo Farms.
Wataalamu 4
wa ufugaji na biashara
Semina imeanza

Ujuzi wa vitendo
Mada 12 kutoka misingi ya fedha hadi teknolojia ya uzazi—vipindi vimeundwa kukupa maarifa unayoweza kutumia shambani mara moja.
Elimu ya fedha na fursa za kilimo-biashara na ufugaji nchini Tanzania.

Kumfahamu ng’ombe bora: Vinasaba, muonekano na matunzo ya ndama.

Inbreeding ya ng’ombe na madhara yake.

Ufugaji bora wa ng’ombe wa maziwa: Mazingira, utunzaji wa maziwa, n.k.

Lishe na ulishaji: Malisho ya kisasa na ya asili.

Kutengeneza saileji (silage).

Utunzaji wa kumbukumbu.

Sababu za utasa kwa ng’ombe.

Namna ya kuongeza ushikaji wa mimba kwa njia ya chupa.

Sayansi ya Embryo Transfer.

Unenepeshaji wa ng’ombe wa nyama.

Ajali na magonjwa: Tahadhari, chanjo na matibabu.

Chukua hatua inayofuata kwa ufugaji wako.
Jiandikishe kwenye semina →
Kila kitu kimeandaliwa
Stationery
Kalamu na daftari kwa kila mshiriki.
Chakula Na Vinywaji
Vitapatikana kwa siku zote mbili.
Cheti Cha Semina
Utapokea cheti baada ya kukamilisha.


Mahali pa semina
Ukumbi upo Mbezi Makonde, ndani ya Mbezi Garden Hotel, Dar es Salaam, katika mazingira tulivu yenye miti na nafasi ya maegesho.
Mahali: Mbezi Garden Hotel, Mbezi Makonde, Dar es Salaam
Hoteli ipo eneo la semina. Bei inaanzia TSh 50,000 kwa usiku na haijajumuishwa kwenye ada ya semina.
Wasiliana na Mbezi Garden: +255 787 280 602Taarifa kamili zitatolewa baada ya semina ya Oktoba 2026.
Ukifika Makonde: Ukumbi upo upande wa kushoto ukitokea Tegeta/Bagamoyo, au upande wa kulia ukitokea Massana/Posta.
Kutana na wawezeshaji
Jifunze kutoka kwa wataalamu wa afya, tija, vinasaba na teknolojia ya ufugaji kutoka Tanzania na Kenya.

Ana shahada ya Animal Health Production and Processing kutoka Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology (JKUAT). Ni daktari wa mifugo anayebobea katika afya, tija na uchakataji wa mazao ya mifugo, akiwa na uzoefu kupitia Biosciences Kenya Ltd.

Ni daktari wa mifugo kutoka Kenya mwenye shahada ya BSc Animal Health Production and Processing kutoka Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology. Kwa zaidi ya miaka minne amefanya kazi na Biosciences Kenya Ltd, kampuni inayobobea katika lishe ya wanyama na utengenezaji wa virutubisho vya madini kwa mifugo. Ana uzoefu katika utengenezaji wa virutubisho, mauzo, masoko na huduma za ugani. Amefundisha wafugaji katika zaidi ya vyama 100 vya ushirika wa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa katika maeneo ya Central na South Rift nchini Kenya.

Ni daktari bingwa binafsi wa wanyama aliyebobea katika ugunduzi wa magonjwa, matibabu na upasuaji unaotokana na magonjwa na ajali, ikiwemo mifupa iliyovunjika na wanyama waliomeza mifuko, kamba au vitu vyenye ncha kali. Ni mhitimu wa Sokoine University of Agriculture na ana zaidi ya miaka 12 ya usimamizi na ushauri wa kitaalamu katika mashamba makubwa nchini, akiwa amefanya upasuaji kwa mamia ya wanyama. Pia ni mfugaji wa ng’ombe wa maziwa na mbwa wa ulinzi kama BM, GSD na Rottweiler. Ofisi yake ipo Kibaha, Mkoa wa Pwani, Tanzania.

Ni mtaalamu wa kiufundi wa mifugo katika URUS Tanzania anayebobea katika reproductive ultrasonography, embryo transfer na artificial insemination. Pia ni mshauri wa mashamba ya mifugo anayesaidia wafugaji kutumia teknolojia za kisasa za kuongeza tija.
Jifunze kutoka kwa wataalamu hawa.
Weka nafasi yako sasa →Video za mafunzo
Fungua vipande vya video vya ufugaji na mafunzo kupitia Instagram na YouTube.
Semina iliyopita
Tazama kumbukumbu za semina yetu iliyopita: washiriki wakijifunza ukumbini na kutembelea shamba.


Nafasi ni chache
Lipa kupitia Selcom Bank na uthibitishe muamala, au weka nafasi yako sasa na ukamilishe malipo baadaye.
Silver Star HallMbezi Garden Hotel, Mbezi Makonde
03–04 Oktoba 2026Tarehe
8:00 AM–6:00 PMMuda
Maswali ya kawaida
Ada ya TSh 150,000 inajumuisha Semina ya siku mbili, stationery, chakula na vinywaji, pamoja na cheti cha Semina.